TEACHER MWAKIGOBE
COMMERCE LESSON NOTES
Sunday, April 3, 2011
TANZANIA NA TIBA YA KIKOMBE.
Nimekaa na kutafakari na kupata msukumo wa kuhoji, hii tiba ya vikombe hatma yake ni ipi? na je asinge anza kujitokeza Mchungaji wa Loliondo wengine wangejitokeza?. Au hawa waganga wengine wamejitokeza baada ya kuona watu wana imani na dawa ya mwaisapile?
Mi nadhani tunatakiwa kuwa makini kwa matukio haya ya kuibuka kwa hawa watu wanaojinadi kuwa wameoteshwa na Mungu kutibu magonjwa sugu. Alipo anza babu wa Loliondo sikuwa na shaka ila sasa wasiwasi unanijia baada ya kusikia eti huko mbeya kuna babu dogo ,nae anatumia kikombe, huko Tabora nako kuna Bobi kikombe na pengine ambapo sijapataja.
hofu yangu ni kuwa hii sasa inaweza ikawa ni fasheni na watu wanataka umaarufu.
pia naishukura sana serikali kufuatilia kwa ukaribu matukio haya ya matibabu ya vikombe.
Ushauri wangu kwa wadau ni kuwa pale Loliondo pajengwe mnara wa kumbukumbu kwani hii sio ishu ndogo.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment